Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 13:53

Watalii waokoloewa Kenya, idadi ya vifo imefikia watu 181 kutokana na mafuriko


Mafuriko yamesababisha vifo na uharibifu mkubwa Kenya April 24, 2024
Mafuriko yamesababisha vifo na uharibifu mkubwa Kenya April 24, 2024

Watalii wameondolewa kwa usafiri wa ndege za helikopta kutoka kwenye hifadhi ya taifa ya Maasai mara nchini Kenya hivi leo Jumatano baada ya darzeni ya hoteli, nyumba za wageni na kambi kujaa maji ya mafuriko kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo.

Nyumba wanazokaa watalii zimejaa maji baada ya mto ulio ndani ya mbuga ya Maasai mara kuvunjika kingo zake mapema hivi leo.

Hifadhi hiyo ya wanyama iliyo kusini magharibi mwa Kenya, ni kituo maarufu sana kwa watalii kwa sababu ya mandhari yake na kuwa na idadi kubwa ya nyumbu ambao wanaotokea Serengeti nchini Tanzania.

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema limewaokoa watu 36 kwa njia ya usafiri wa anga na wengine 25 kwa njia ya barabara.

Serikalli ya kaunti ya Narok imesema imepeleka helikopta mbili kuwabeba watu wanaoondolewa katika eneo hilo la hifadhi.

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko nchini Kenya imefikia 181.

Kulingana na shirika la kutoa msaada la msabala mwekundu, maelfu ya watu wamekoseshwa makazi.

Watu 48 walifariki Mai Mahiu, katikati mwa Kenya na shughuli za uokoaji na kutafuta miili inaendelea kwa kutumia mbwa wa kunusa.

Maafisa wa shirika la msalaba mwekundu wanaendelea kuwasaidia wakaazi wa Kitengela, kilomita 33 kutoka Nairobi ambao nyumba zao zimejaa maji, pamoja na kuwaokoa watalii katika mji wa Narok, kilomita 215 kutoka Nairobi.

Watu kadhaa wamefariki Tanzania na Burundi kutokana na mafuriko ambayo pia yameharibu nyumba, barabara, daraja na miundo msingi mingine Afrika mashariki.

Forum

XS
SM
MD
LG