Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 11:10

Wabunge wa Georgia wapigana bungeni


Polisi wakikabiliana na mtu aliyekuwa akiandamana karibu na bunge, Tbilisi, Georgia May 1, 2024
Polisi wakikabiliana na mtu aliyekuwa akiandamana karibu na bunge, Tbilisi, Georgia May 1, 2024

Vurugu zimetokea katika bunge la Georgia wakati wabunge waliokuwa wakijadili mswaada unaojulikana kama mawakala wa n je, ambao umesababisha maandamano kwa wiki kadhaa, na kupelekea Polisi kufanya msako mkali.

Televisheni ya Georgia imeonyesha vurugu ndani ya bunge wakati wa kikao.

Mmoja wa mbunge anayeiunga mkono serikali alionekana akirusha kitabu kuelekea upande walipokuwa wabunge wa upinzani, huku wabunge wengine wakipaaza sauti na kusukumana.

Mswaada huo umepelekea kuongezeka kwa ghasia katika bunge la Georgia ambalo hushuhudia vurugu kila mara.

Maafisa wa usalama wa Georgia walitumia maji, gesi ya kutoa machozi na vilipuzi dhidi ya waandamanaji nje ya bunge, jumanne, na kuongeza msako baada ya wabunge kujadili mswaada huo wa mawakala wa nje ya nchi ambao umetajwa na upinzani pamoja na n chi za magharibi kuwa kandamizi na wenye ushawishi wa Russia.

Polisi wanawazuia watu 63 na polisi sita wamejeruhiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG