Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 11:10

Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi yaibua dharura ya kujitolea upya kwa  haki za kijamii

Wafanyakazi wa Wizara,Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi wakipita mbele ya Jukwaa Kuu kutoa ujumbe kuhusiana na masuala mbalimbali ya Wafanyakazi. Sherehe zimefanyika kitaifa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 Mei 2024. - Ikulu

Mwaka huu Sherehe za Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi zina hisia ya dharura ya kujitolea upya kwa haki za kijamii, wakati tunapopitia kipindi kigumu, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya haraka katika sehemu za kazi kutokana na maendeleo ya teknolojia.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Kazi Duniani, ILO inasema: "Leo, tunaposimama pamoja kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi tunakumbushwa kuhusu historia iliyojitosheleza na umuhimu wa siku hii; siku ambayo ni ishara ya mapambano na mafanikio ya wafanyakazi duniani kote. Siku ambayo inahusiana na dhamira yetu ya pamoja ya kuendeleza haki na mazingira bora ya wafanyakazi kokote walipo.”

"Changamoto hizi siyo tu zimejaribu ustahmilivu wetu lakini pia zimesisitiza umuhimu wa juhudi za za pamoja katika kuhamasisha maslahi ya wafanyakazi katika sekta zote, " iliongeza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema Bangladesh, imepiga hatua kubwa katika katika ukuaji wa uchumi na iko katika kilele cha mpito wa historia, na kusonga mbele katika kujikwamua kutoka kuwa nchi inayoendelea (LDC) ifikapo mwaka 2026.

Mafanikio haya ni ushahidi wa kazi ngumu na ustahmilivi wa watu wake, ikwemo idadi kubwa ya nguvu kazi yake, ambayo ni uti wa mgongo katika ukuaji wa uchumi wa taifa hilo, ilieleza taarifa hiyo.

ILO inasema wakati dunia ikiadhimisha mafanikio ya kihsitoria, "ni lazima tushughulikia suluhu ya changamoto zinazoendelea na zinazojitokeza ambazo huwakabili wafanyakazi kila siku."

Makamu wa Rais Tanzania Mhe Philip Mpango akiwapungia mkono Wafanyakazi wakati wakipita mbele ya Jukwaa Kuu katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 Mei 2024. - Ikulu

Taarifa ya ILO inaeleza kuwa: “Wakati tukikabiliana na mustakbali wetu, turudie kutoa ahadi mpya kusimamia haki za kijamii, kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi unafanikiwa kuboresha hali ya maisha na mazingira bora zaidi ya sehemu za kufanyia kazi kwa wote.”

“Pia tujenge ushirikiano imara na tuimarishe kuwepo mazungumzo kati yetu, kwani ni kupitia hatua za pamoja tu na maelewano ya pande mbili tutaweza kuzitatua changamoto zilizoko mbele yetu, ripoti hiyo imeeleza.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Kazi Duniani, ILO.

Forum

XS
SM
MD
LG