Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 02:22

Makombora ya Russia yameharibu mfumo wa umeme wa Ukraine


Moshi ukivuka baada ya makombora kuanguka Chasiv Yar, Donetsk May 3 2024
Moshi ukivuka baada ya makombora kuanguka Chasiv Yar, Donetsk May 3 2024

Maafisa wa Ukraine wamesema leo Jumatano kwamba mashambulizi kadhaa ya anga yakiwemo makombora 55 na ndege zisizokuwa na rubani 21 yameharibu kituo cha kuzalisha umeme katika mkoa wa Lviv, magharibi mwa Ukraine.

Kampuni kubwa binafsi ya kuzalisha umeme DTEK, imesema kwamba makombora ya Russia yamesababisha uharibifu mkubwa kwa mitambo yake mitatu kati ya sita nchini Ukraine.

Gavana wa Lviv Maksym Kozytskyi, ameandika ujumbe wa Telegram kwamba makombora ya Russia yameharibu vituo vya kuzalisha umeme katika wilaya ya Chervonohrad na katika wilya ya Stryi.

Hakuna ripoti za vifo.

Kwingineko Gavana wa Korovohrad ameripoti kifo cha mtu mmoja na 13 kujeruhiwa, pamoja na nyumba kadhaa kuharibiwa katika mashambulizi ya Russia.

Maafisa katika Vinnytsia vile vile wameripoti mashambulizi ya makombora ya Russia ambayo yameharibu miundo mbinu muhimu.

Jeshi la anga la Ukraine limesema kwamba mfumo wake wa ulinzi umeharibu makombora 39 kati ya 55 yaliyorushwa, na ndege zisizokuwa na rubani 20 kati ya 21.

Forum

XS
SM
MD
LG