Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 14:53

Juhudi za kumaliza vita vya Gaza zinaendelea


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akiondoka uwanja wa ndege wa Joint Base Andrews akielekea Saudi Arabia kwa juhudi za kidiplomasia kwa ajili ya Gaza April 28, 2024.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akiondoka uwanja wa ndege wa Joint Base Andrews akielekea Saudi Arabia kwa juhudi za kidiplomasia kwa ajili ya Gaza April 28, 2024.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Stephane Sejourne amewasili Cairo, Misri kama sehemu ya juhudi za kidiplomasia kutafuta makubaliano ya sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas.

Sejourne atakutana na maafisa wa Misri katika ziara yake ambapo pia ataitembelea Lebanon, Saudi Arabia na Israel.

Mji wa Cairo umekuwa mwenyeki wa mikutano ya mashauriano yanayohusisha wapatanishi kutoka Marekani, Misri na Qatar ambapo wamepokea mapendekezo namna ya kumaliza vita vya Gaza.

Mapendekezo yanataka vita kusitishwa kwa wiki kadhaa, kuachiliwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas, kuachiliwa wafungwa wa Palestina wanaozuiliwa Israel na kuongeza misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza.

Baada ya kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Isreal Benjamin Netanyahu, Sejourne amesema kwamba sera ya Ufaransa inasalia kwamba ni lazima mateka waachiliwe huru, makubaliano ya kusitisha vita yasainiwe na mazungumzo ya kumaliza vita yafanyike Lebanon.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken nayo yupo kwenye ziara ya kidiplomasia mashariki ya kati, kutafuta namna ya kumaliza vita. Anatarajiwa kufanya mazungumzo na maafisa wa Israel leo Jumatano.

Jeshi la Isreael limesema leo kwamba limetekeleza mashambulizi usiku wa kuamkia leo dhidi ya kundi la Hezbollah, kusini mwa Lebanon.

Forum

XS
SM
MD
LG