Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 10:07

Baraza la mpito Haiti lagawanyika baada ya uteuzi wa Waziri Mkuu mpya


Baadhi ya viongozi wa kisiasa Haiti
Baadhi ya viongozi wa kisiasa Haiti

Hatua iliyoshangaza wengi ya kutangazwa kwa waziri mkuu mpya wa Haiti Jumanne, sasa inaligawanya baraza la mpito, lililoundwa hivi karibuni na kupewa jukumu la kuchagua viongozi wapya wa nchi hiyo ya Caribbean, yenye matatizo kutokana na uhalifu wa magenge.

Wajumbe wanne kati ya saba walio na mamlaka ya kupiga kura walisema Jumanne kwamba wamemchagua Fritz Bélizaire kama waziri mkuu. Wananchi wengi wa Haiti walishangazwa na tamko lao na muungano wa kisiasa ambao haukutarajiwa.

Wanachama wa baraza wanaompinga Bélizaire sasa wanatafakari nini cha kufanya, ikiwemo uwezekano wa kupinga uamuzi huo au kujiuzulu kutoka kwa baraza hilo.

Bélizaire aliwahi kuwa waziri wa michezo wa Haiti wakati wa uongozi wa rais wa pili wa nchi hiyo, René Préval, kuanzia 2006 hadi 2011.

Forum

XS
SM
MD
LG